Wednesday, 14 January 2015

image


ict in education


mwalimu na wanafunzi wake

bi sharifa akizungumza na wanafunzi wake katika skuli ya umoja uzini alipokua mazoezini

eeeee

bbbbbgggbvcsdmmmmmmmmmmmmmmmkjwhdjka,sbnbm,,,,m.msg

MAPINDUZI CUP FINAL


Akitokea bench mnamo dakika ya 90 kuchukua nafasi ya mlinda mlango Peter Manyika kipa mkongwe wa wekundu wa msimbazi (Simba)  Ivo Mapunda amefanikiwa kuipa timu yake ubingwa wa tatu katika mashindano ya kombe la mapinduzi baada ya kupangua mkwaju wa mwisho wa penalti wa Vicent Barnabas.
Simba imetwaa ufalme huo wa mashindano ya tisa ya mapinduzi cup baada ya kuibuka na ushindi wa penalt  4-3 dhidi ya timu ya Mtibwa sugar katika mchezo wa fainal uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini Unguja mnamo majira ya saa 2 na robo usiku wa kuamkia leo ambapo awali katika dakika 90 timu hizo zimetoka suluhu yakutokufungana.
Akizungumza mara baada ya mchezo huo kocha wa timu ya Mtibwa sugar Mecky Mekisime amesema kwa sasa macho na akili yao yote wanaielekeza katika ligi kuu ya Tanzania bara nakuelezea kuwa mashindano hayo yamewapa mazoezi yakutosha vijana wake na kupongeza kiwango kilichooneshwa na timu yake katika mchezo huo wa faianl.
Insert mtibwa………………….
Kwa upande wake kocha wa Simba Goran Kopunovic  amesema mashindano hayo yamemfanya kuwajua wachezaji wake na kuhakikisha anayafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwa timu yake katika mashindano hayo ili kufanya vyema katika michezo iliyobakia ya ligi kuu ya Tanzania bara nakusifia mchezo ulioneshwa na timu zote mbili.
Insert simba………………
Akizungumza na ABM RADIO rais wa chama cha mpira wa miguu Tanzani (TFF) Jamal Malinzi amesema mashindano hao yamekuwa na ushindi mkubwa sambamba na kufichua vipaji vya wachezaji wanaocheza ligi kuu ya Zanzibar huku akiwapongeza wapenda soka wote waliojitokeza katika mashindano hayo.
Insert jamal…………………
Akizungumza na ABM RADIO kipa bora wa mashindano hayo ya tisa ya mapinduzi  Said Mohammed wa Mtibwa Sugar amesema mashindano hayo yamempa changamo nyingi ambazo atazifanyia kazi ili kutimiza malengo yake na kusema mashindano hayo yamekuwa mazuri.
Insert……………..
Nae mchezaji wa bora wa mashindano hayo beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ameelezea kufurahishwa kwa kutawazwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo nakuezea kuwa mchezo huo wa fainal ulikuwa nzuri na ushindani.
Insert mchezaji bora…………………

Simba Simba imekabidhiwa kitita cha Sh milioni 10 kombe pamoja na medali za dhahabu wakati washindi wa pili Mtibwa Sugar wameondoka na Sh milioni 5 pamoja na medali za fedha ambapo katika mashindano hayo kipa  bora ameteuliwa Said Mohammed wa Mtibwa Sugar,mchezaji bora wa mashindano hao ya tisa akiteuliwa beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde huku tunzo ya mfungaji bora ikienda kwa Simon Msuva wa Yanga ambaye alifunga mabao manne ambapo washindi hao watatu kila mmoja amezawadiwa king’amuzi cha Azam TV huku rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dr. Ali Muhamed Shein akikabidhi zawadi kwa washindi.