Wednesday, 14 January 2015
MAPINDUZI CUP FINAL
Akitokea
bench mnamo dakika ya 90 kuchukua nafasi ya mlinda mlango Peter Manyika kipa mkongwe wa wekundu
wa msimbazi (Simba) Ivo Mapunda amefanikiwa
kuipa timu yake ubingwa wa tatu katika mashindano ya kombe la mapinduzi baada ya
kupangua mkwaju wa mwisho wa penalti wa Vicent Barnabas.
Simba
imetwaa ufalme huo wa mashindano ya tisa ya mapinduzi cup baada ya kuibuka na
ushindi wa penalt 4-3 dhidi ya timu ya
Mtibwa sugar katika mchezo wa fainal uliovurumishwa katika dimba la Amani mjini
Unguja mnamo majira ya saa 2 na robo usiku wa kuamkia leo ambapo awali katika
dakika 90 timu hizo zimetoka suluhu yakutokufungana.
Akizungumza
mara baada ya mchezo huo kocha wa timu ya Mtibwa sugar Mecky Mekisime amesema
kwa sasa macho na akili yao yote wanaielekeza katika ligi kuu ya Tanzania bara
nakuelezea kuwa mashindano hayo yamewapa mazoezi yakutosha vijana wake na
kupongeza kiwango kilichooneshwa na timu yake katika mchezo huo wa faianl.
Insert
mtibwa………………….
Kwa upande
wake kocha wa Simba Goran Kopunovic amesema
mashindano hayo yamemfanya kuwajua wachezaji wake na kuhakikisha anayafanyia
kazi mapungufu yaliyojitokeza kwa timu yake katika mashindano hayo ili kufanya
vyema katika michezo iliyobakia ya ligi kuu ya Tanzania bara nakusifia mchezo
ulioneshwa na timu zote mbili.
Insert
simba………………
Akizungumza
na ABM RADIO rais wa chama cha mpira wa miguu Tanzani (TFF) Jamal Malinzi
amesema mashindano hao yamekuwa na ushindi mkubwa sambamba na kufichua vipaji
vya wachezaji wanaocheza ligi kuu ya Zanzibar huku akiwapongeza wapenda soka
wote waliojitokeza katika mashindano hayo.
Insert
jamal…………………
Akizungumza
na ABM RADIO kipa bora wa mashindano hayo ya tisa ya mapinduzi Said Mohammed wa Mtibwa Sugar amesema
mashindano hayo yamempa changamo nyingi ambazo atazifanyia kazi ili kutimiza
malengo yake na kusema mashindano hayo yamekuwa mazuri.
Insert……………..
Nae mchezaji
wa bora wa mashindano hayo beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim Mbonde ameelezea
kufurahishwa kwa kutawazwa kuwa mchezaji bora wa mashindano hayo nakuezea kuwa
mchezo huo wa fainal ulikuwa nzuri na ushindani.
Insert
mchezaji bora…………………
Simba Simba
imekabidhiwa kitita cha Sh milioni 10 kombe pamoja na medali za dhahabu wakati
washindi wa pili Mtibwa Sugar wameondoka na Sh milioni 5 pamoja na medali za
fedha ambapo katika mashindano hayo kipa bora ameteuliwa Said Mohammed wa Mtibwa Sugar,mchezaji
bora wa mashindano hao ya tisa akiteuliwa beki wa kati wa Mtibwa Sugar, Salim
Mbonde huku tunzo ya mfungaji bora ikienda kwa Simon Msuva wa Yanga ambaye
alifunga mabao manne ambapo washindi hao watatu kila mmoja amezawadiwa
king’amuzi cha Azam TV huku rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi Dr. Ali Muhamed Shein akikabidhi zawadi kwa washindi.
Subscribe to:
Posts (Atom)